Skip to main content

‏ MUNGU, KIZA NA ULIMWENGU.(100)-Mashairi Ya Rangimoto

Mashairi Ya Rangimoto MUNGU, KIZA NA ULIMWENGU.(100)
1.
Naomba kusimulia,
Mambo yanayo tukia,
Katika yetu dunia,
Usiku ukiingia.
2.
Kiza kikiinukia,
Wasiwasi huningia,
Sababu usiku njia,
Kifo anayo tumia.
3.
Kuna vitu nawajuza,
Vyaishi katika kiza,
Endapo mkichunguza,
Nanyi mtashuhudia
4.
Hivyo vitu vimejaza,
Mambo ya mauzauza,
Na mengi ya kushangaza,
Katika yetu dunia.
5.
Kuna aitwaye MUNGU,
Yeye wa tangu na tangu,
Kaumba wote ulimwengu,
Vitu ndani kavitia.
6.
Ardhi saba na mbingu,
Theluji nawo ukungu,
Mvua na yake mawingu,
Sayari na zake njia.
7.
Kaumba chungu na tamu,
Edeni na Jahanamu,
Unduli na ukarimu,
Amani na vita pia.
8.
Ujinga na ufahamu,
Ukaidi na nidhamu,
Kupungua na kutimu,
Mwenyewe kajifanyia.
9.
Pia wapo malaika,
Kaumba aso shirika,
Watiifu bila shaka,
Peke wamtumikia.
10.
Idadi yao hakika,
Anaijua Rabuka,
Ela lilothibitika,
Wingi wametuzidia.
11.
Wako wakubwa wanne,
Singoji siku nyingine,
Leo miye niwanene,
Furusa naitumia.
12.
Miye nataka muone,
Twende sote siachane,
Niwape habari nene,
Mketi kwa kutulia.
13.
Wa kwanza ni Mikaili,
Mwenye upanga mkali,
Kila panapo kitali,
Majeshi huyapa njia.
14.
Mbawa zake sio mbili,
Ila nyingi kweli kweli,
Idadi yake kamili,
Anayejua Jalia.
15.
Mbawa zake ni maalfu,
Zimejipanga kwa safu,
Huyu bwana hana khofu,
Vitani akiingia.
16.
Alipofanya machafu,
Na kumuasi Raufu,
Ibilisi mpotofu,
Panga alimshikia.
17.
Sasa nataja wa pili,
Si mwingine Jibrili,
Huwandea Marasuli,
Ujumbe kuwapatia.
18.
Zijaa nyingi dalili,
Hawakufanya halali,
Kwa umma iwe batili,
Bila ya kumsikia.
19.
Alianza kwa Adamu,
Baba yetu binadamu,
Akitumwa na Rahimu,
Wahayi kumpatia.
20.
Tamati ikawa zamu,
Kutoka Bani Hashimu,
Alipatiwa salamu,
Kama walotangulia.
21.
Zimeshakatika zama,
Nazo hazirudi nyuma,
Zimepita pia umma,
Wenzangu nawaambia.
22.
Mwenyenzi alimtuma,
Mtume kwa kila umma,
Afundishe yalo mema,
Na kila nzuri tabia.
23.
Wa tatu Israfili,
Hanazo nyingi shughuli,
Anasubiri kauli,
Panda kutupulizia.
24.
Yuko huyo Ziraili,
Waja humwona katili,
Mtu akifa mahali,
Juwa keshampitia.
25.
Kuna viumbe majini,
Baadhi ni mashetani,
Wanajazana njiani,
Wapitao huvamia,
26.
Wameumbwa na Manani,
Waishi ulimwenguni,
Kwa sheria na kanuni,
Bila kuzipuuzia.
27.
Wapo majini katili,
Kwao wao si muhali,
Kusababisha ajali,
Mamia kuangamia.
28.
Wapo wenye afadhali,
Wanaotawala mwili,
Wataka lile na hili,
Umasikini watia
29.
Mara pete ya dhahabu,
Yenye harufu ya subu,
Majini huleta tabu,
Wenzangu nawaambia.
30.
Ati nguo za kasabu,
Ama atake kababu
Majini wanadhurubu,
Lao sipowafanyia.
31.
Wapo majini mahaba,
Wanozama kwenye huba,
Kuwa nao ni adhaba,
Penzi hukuvurugia.
32.
Ndotoni akikubeba,
Hilo jini la mahaba,
Taamka na janaba,
Nguo mejichafulia
33.
Wapo wengine vibubu,
Mabingwa wa kudhurubu,
Ongea yao ni tabu,
Ishara wanatumia
34.
Wapo wale matabibu,
Hutazama kwa ghaibu,
Maradhi yanokusibu,
Kisha wanakutibia.
35.
Msambe ni ukilaza,
Kwa haya ninoeleza,
Lau mngapeleleza,
Shaka msingeitia.
36.
Kuna aitwaye KIZA,
Huyu ndiye aniliza,
Sababu yeye awaza,
Kuiyayusha dunia.
37.
MUNGU ataangamizwa,
Kabisa atapotezwa,
Vyote vilivyotengezwa,
Naye havitasalia.
38.
Ulimwengu utamezwa,
Sio kama kumalizwa,
Nabaki ninatatizwa,
KIZA nikimfikiria
39.
Kabla ya kuumbwa siku,
Mchana hata usiku,
Kutupu huko na huku,
KIZA alijikalia.
40.
Kaja tolewa mkuku,
Na maguvu ya sumaku,
MUNGU kaweza kupiku,
KIZA akamfungia.
41.
Mara kukalia puu,
Kumbe kishindo kikuu,
KIZA akapazwa juu,
BING BANG ‘katokea.
42.
Katika wakati huu,
Zikaumbwa nuru kuu,
Na malaika wakuu,
Pumzi wakajipatia.
43.
Mikaeli Israfili,
Ziraili Jibrili,
Walishiriki kitali,
Cha KIZA kumfungia.
44.
Leo nawapa ukweli,
Munabudi kukubali,
Hii vita ya awali,
Kabisa nawaambia.
45.
Ba’da kiza kufungiwa,
Ulimwengu kuzaliwa,
Mengine mengi yakawa,
Kwa uwezo wa Jalia.
46.
Gerezani ‘lipotiwa,
Ngomeze zikatwaliwa,
Yale aliyoachiwa,
Mungu ayafikiria.
47.
Kila saa na dakika,
Ulimwengu watanuka,
Unazidi kuyateka,
Sehemu zilosalia.
48.
Yakiwa yanatendeka,
KIZA jela ateseka,
Huku akihangaika,
Kifungoni kujitoa.
49.
Kuna jambo la muhimu,
Kuhusu hiyo sehemu,
Funguo zake adhimu,
Ni madhambi nawambia.
50.
Watu wapenda haramu,
Dhambi zimekuwa tamu,
Ela waja tufahamu,
KIZA twamfungulia.
51.
KIZA jela ametiwa,
Na cheni kazungushiwa,
Awaza na kuwazuwa,
Jinsi ya kujitokea.
52.
Rusifa munamjuwa,
Ibilisi halikuwa,
Hilo jina amepawa,
KIZA lipomfikia.
53.
Si ahera si kuzimu,
Si ulimwenguni humu,
Ya siri hiyo sehemu,
KIZA alipofungiwa.
54.
Alipoumbwa Adamu,
KIZA katuma salamu,
Kwa nguvu zake adhimu,
Rusifa kamfikia.
55.
KIZA fika alijuwa,
Rusifa tamuelewa,
Jela atalifunguwa,
Dhambini akiingia.
56.
Paukwa kisha pakawa,
Adamu kapokelewa,
Na wote wakaambiwa,
Mtu kumsujudia.
57.
Ibilisi akakaa,
Kama aliyeduwaa,
Na kisha akakataa,
Mtu kumsujudia.
58.
Kumbe tayari jamaa,
KIZA alishamvaa,
Kaziye akaitwaa,
Jela kumfungulia.
59.
Mia sita na sitini,
Na sita ziongezeni,
Makomeo ya langoni,
KIZA alipofungiwa.
60.
Tunda la mti wa shani,
Katikati ya bustani,
Inayoitwa Edeni,
Ndiyo komeo la kwanza.
61.
Sio tunda la kuliwa,
Na wala kusumbuliwa,
Adamu kazuiliwa,
Mti kuukaribia.
62.
Wanawake hawahawa,
Mama yao ndio Hawa,
Ndiye alorubuniwa,
Mti kuukaribia.
63.
Adamu alikosea,
Mti kuusogelea,
Tunda akajimegea,
Na uchi akabakia.
64.
Mambo yaliyotokea,
Hawa hakutegemea,
Rusifa kajiendea,
Msala kawaachia.
65.
Lango lika tikisika,
Baada tunda kulika,
Komeo likakatika,
La kwanza nawaambia.
66.
MUNGU akasikitika,
Laana akatamka,
Hawa mimba utashika,
Kwa uchungu utazaa.
67.
Adamu utatafuta,
Kwa ugumu utapata,
Utayachimba matuta,
Mbegu utajipandia.
68.
Riziki ni vutavuta,
Kukosa pia kupata,
Jasho jingi tajifuta,
Kivulini kitulia.
69.
Alipanga tuoane,
Duniani tujazane,
Ela kwa njia nyingine,
Siyo tunayotumia.
70.
Lengo lake tupendane,
Na sote turidhiane,
Kwa dhati tushikamane
Sema KIZA kavuruga.
71.
Siku hazikwenda mbali,
Akazaliwa Habili
Alikuwa ni wa pili,
Kakaye ndiye Kaini.
72.
Kuuliwa kwa Habili,
Na Kaini kikatili,
Komeo nambari mbili,
Likawa limefunguka
73.
Damu ya kwanza tiifu,
Toka kwa mtakatifu,
Mwenye kuumcha Raufu,
Ndiyo komeo la pili.
74.
Dunia ‘kajaa khofu,
Kwa kuzidi upotofu,
Waja ‘kifanya uchafu,
Rusifa afurahia.
75.
Miaka ikakatika,
Adamu ‘lipokauka,
Ikatokea gharika,
Nuhu akaokolewa.
76.
Mungu alilazimika,
Kuleta ile gharika,
Na ilipomalizika,
KOMEO likafunguka.
77.
Sita sitini na sita,
Kuyafungua ni vita,
Yapo sitini na sita,
Kwayo KIZA atatoka.
78.
Ibilisi hatawata,
Njia kuzitafuta,
Hizo zote sita sita,
Aweze kuzifunguwa.
79.
Naye MUNGU akazana,
Malaika wapambana,
Kwa juhudi kubwa sana,
Funguo kushikilia.
80.
Kumwabudu Subhana,
Kumuhofu Maulana,
Yote yanasemekana,
Huyapa nguvu milango.
81.
Milango itafunguka,
Kwa kumuasi Rabuka,
Pia itadhibitika,
Kwa kumtii Jalia.
82.
Naomba kueleweka,
Sala saumu na Zaka,
Yote yanahitajika,
Ili KIZA kuzuwia.
83.
Pia kuyafanya mema,
Usiku na kutwa nzima,
Kutii baba na mama,
Bila kuvunja sheria.
84.
Hayo ataka Karima,
Waja wake tuwe wema,
Ili tushinde nakama,
Ya KIZA kumuwachia.
85.
Jambo fulani ni baya,
Kulifanya ni khatiya,
Ushawahi fikiriya,
Kwanini lisiwe jema?
86.
Hili zuri lile baya,
Kama ukizingatiya,
Fikra zitakuambiya,
Haya yote ni majina.
87.
Hivyo basi ni kweli,
Haramu au batili,
Hutegemea kauli,
Ya YULE aloamua.
88.
Ametutaka Jalali,
Tufanye yalo halali,
Ila budi tukubali,
KIZA ana yake pia.
89.
Kinyume cha haya yote,
Ukiyaona popote,
Katika sura yoyote,
Juwa kwa KIZA halali.
90.
Hali imekuwa tete,
Kuna vuta nikuvute,
Sasa ulimwengu wote,
Kwa vita watikisika.
91.
Ukisoma Biblia,
Quran ukipitia,
Humo utayakutia,
Baadhi niliyosema.
92.
Sio mbaya yangu nia,
Haya kuwaandikia,
Ruhusa kuniwachia,
Lolote nilopotosha.
93.
Hayupo alokamili,
Ela ni Mola Jalali,
Hachoki wala halali,
Maumbile kukosea.
94.
Miye kiumbe dhalili,
Rabbi nakuomba hili,
Nipa thabiti kauli,
Leo na kesho qiyama.
95.
Sikuandika kwa pato,
Nimesikia mguto,
Nikaufuata wito,
Utendi kuwatungia.
96.
Ndimi miye Bwana Dotto,
Ni mwana wa Rangimoto,
Bado ningali mtoto,
Nikosapo munionye.
97.
Kijana wenu kipenzi,
Ningali ni mwanagenzi,
Milele nitawaenzi,
Na hadhi kuwapatia.
98.
Ninamuomba Mwenyenzi,
Mkaa kiti cha enzi,
Kwa mahaba na mapenzi,
Vita tuweze kushinda.
99.
Haya niliyowapasha,
Mimi yaniogopesha,
Ndio hasa yanitisha,
Usiku ukiingia.
100.
Beti miya zinachosha,
Niloandika yatosha,
Naomba kukamilisha,
Kwa madhambi kutubia.

30 January 2017 Jumatatu.
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whats app 0622845394 Morogoro.

Comments

Popular posts from this blog

Mona Farouk reveals scenes of "scandalous video"Egyptian actress Mona Farouk appeared on

Mona Farouk reveals scenes of "scandalous video"Egyptian actress Mona Farouk appeared on Monday in a video clip to discuss the details of the case she is currently facing. She recorded the first video and audio statements about the scandalous video that she brings together with Khaled Youssef.Farouk detonated several surprises, on the sidelines of her summons to the Egyptian prosecution, that Khalid Youssef was a friend of her father years ago, when she was a young age, and then collected a love relationship with him when she grew up, and married him in secret with the knowledge of her parents and her father and brother because his social status was not allowed to declare marriage .Muna Farouk revealed that the video was filmed in a drunken state. She and her colleague Shima al-Hajj said that on the same day the video was filmed, she was at odds with Shima, and Khaled Yusuf repaired them and then drank alcohol.She confirmed that Youssef was the one who filmed the clips whil...

الحلقة 20 هنادي المطلقة والمحلل (ماذا قال كتاب العرب في هنادي)-----------Khalid Babiker

• الجنس شعور فوضوي يتحكم في الذات والعقل . وله قوة ذاتية لا تتصالح إلا مع نفسها . هكذا قال أنصار المحلل الحلقة 20 هنادي المطلقة والمحلل (ماذا قال كتاب العرب في هنادي) أول طريق عبره الإنسان هو طريق الذكر . بعدها شهق وصرخ . تمرغ في الزيت المقدس . وجرب نشوة الأرغوس . عاجلا أم آجلا سيبحث عن هذا الطريق ( كالأسماك تعود إلى أرض ميلادها لتبيض وتموت ) . وسيعبره . سيعبره بحثا عن الديمومة . وسيشهق وسيضحك . لقد جاء إليه غريبا . سيظل بين جدرانه الدافئة غريبا . وحالما يدفع تلك الكائنات الحية الصغيرة المضطربة في الهاوية الملعونة سيخرج فقيرا مدحورا يشعر بخيانة ما ( ..... ) . لن ينسى الإنسان أبدا طريق الذكر الذي عبره في البدء . سيتذكره ليس بالذاكرة وإنما بالذكر . سيعود إليه بعد البلوغ أكثر شوقا وتولعا . ولن يدخل فيه بجميع بدنه كما فعل في تلك السنوات التي مضت وإنما سيدخل برأسه . بعد ذلك سيندفع غير مبال بالخطر والفضيحة والقانون والدين . الله هناك خلف الأشياء الصغيرة . خلف كل شهقة . كل صرخة مندفعا في الظلام كالثور في قاعة المسلخ . الله لا يوجد في الأشياء الكبيرة . في الشرانق . في المح . ينشق فمه . تن...

Trusting Liar (#5) Leave a reply

Trusting Liar (#5) Leave a reply Gertruida is the first to recover.  “Klasie… ?” “Ag drop the pretence, Gertruida. You all call me ‘Liar’ behind my back, so why stop now? Might as well be on the same page, yes?” Liar’s face is flushed with anger; the muscles in his thin neck prominently bulging. “That diamond belongs to me. Hand it over.” “What are you doing? Put away the gun…” “No! This…,” Liar sweeps his one hand towards the horizon, “…is my place.  Mine!   I earned it! And you…you have no right to be here!” “Listen, Liar, we’re not the enemy. Whoever is looking for you with the aeroplane and the chopper….well, it isn’t us. In fact, we were worried about you and that’s why we followed you. We’re here to help, man!” Vetfaan’s voice is pleading as he takes a step closer to the distraught man. “Now, put down the gun and let’s chat about all this.” Liar hesitates, taken aback after clearly being convinced that the group  had hostile intentions. “I…I’m ...